Binadamu hutegemeana na viumbe wengine. Huingiliana kwa njia changamano, katika mfumo unaotegemeana ambapo kila mmojawapo huwa na kazi muhimu. Sehemu moja ikibadilishwa–au ikiondolewa–mfumo mzima unaathiriwa, na matokeo yanaweza kuwa chanya au ghasi.

Suluhu ni mazingira

Mazingira huzuia na kukabiliana na baadhi ya changamoto anazokumbana nazo mwanadamu. Husafisha hewa tunayopumua, husafisha maji tunayokunywa, na hutupa aina mbalimbali ya vyakula tunavyohitaji ili kuwa na siha njema na kukabiliana na magonjwa. Husaidia watafiti wa masuala ya afya kuelewa fiziolojia ya binadamu; na kutupa vifaa vya kutumia kutengeneza madawa. Pia, husaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuhifadhi kaboni, kupunguza uchafuzi wa hewa na kupunguza joto mijini.

Changamoto ni binadamu

Shughuli za binadamu zimepunguza bayoanwai na kuathiri makazi ya wanyamapori kwa kiwango kikubwa. Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, idadi ya watu duniani imeongezeka mara dufu; uchumi wa kimataifa umeimarika karibu mara nne zaidi na biashara ya kimataifa imeongezeka takribani mara kumi zaidi. Sasa, Itachukua uongezekaji wa dunia na kuwa 1.6 ili kuweza kukidhi mahitaji ya binadamu kila mwaka.; na aina nyingi ya viumbe wamo hatarini zaidi kuangamia.

Bayoanuai na virusi vya korona

Kuzuka kwa visusi vya COVID-19 ni ishara tosha kuwa tukiharibu bayoanuai, tunaharibu mfumo ambao huwezesha binadamu kuishi. Ubayoanuai wa mifumo ya ekolojia hufanya kuwa vigumu kwa vijidudu vinavyosababisha magongwa kuenea haraka au kuwa sugu; kwa upande mwingine, uharibifu wa bayoanuai hutoa fursa kwa vijidudu vinavyosababisha magongwa kuenea kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu

Matendo ya binadamu kama vile ukataji wa miti, kukalia makazi ya wanyamapori, kulima kupindukia na ongezeko la mabadiliko ya tabianchivimeathiri uwezo wa mazingira ulio dhaifu. Tumebadilisha mfumo ambao ungetulinda kiasilia, na tumesababisha hali ambazo zinawezesha vijidudu vinavyosababisha magongwa kama vile virusi vya korona kuenea.

Sasa, inaaminika kuwa visa takribani bilioni moja vya magonjwa na mamilioni ya vifo hutokea kila mwaka kutokana na magonjwa yanayosababishwa na virusi vya aina ya korona, natakribani asilimia 75 na magonjwa yote ambukizi yanayozuka hutoka kwa wanyama, kumaanisha kuwa binadamu huambukizwa kutoka kwa wanyama Mazingira yanatupa ujumbe.

Ni wakati wa Mazingira

Janga la COVID-19 ni fursa ya kutafakari kuhusu jinsi tunavyohusiana na mazingira na kufanya maamuzi yatakayoboresha dunia kwa kujali mazingira. Kukabiliana na magonjwa yanayozuka kutokana na wanyama kunahitaji kukabiliana na chanzo chake kikuu, haswa, athari zinatokana na shughuli za binadamu. Wakati ambapo idadi ya watu duniani inaelekea kufika bilioni 10, tunapaswa kuelewa maingiliano kati ya viumbe wote na kuelewa kuwa hufanya kazi kwa kutegemeana kama mfumo mmoja. Ni wakati wa kubadili mienendo yetu kwa mazingira na kuyafanya mazingira nguzo ya uamuzi wetu.