UBORESHAJI WA MIFUMO YA EKOLOJIA

HALI HALISI

  • Uboreshaji na masuluhisho mengine ya kiasili unaweza kufikisha theluthi moj, juhudi zinahitajika kufika mwaka 2030 ili kudumisha joto duniani chini ya nyuzijoto 2 na kwa wakati uo huo kusaidia jamii na chumi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Griscom et al., 2017Kapos et al., 2019)
  • Kurejesha asilimia 15 ya ardhi ambayo matumizi yalibadilishwa katika hali yake halisi kunaweza kuzuia asilimia 60 ya spishi zinazotarajiwa kuangamia. (Strassburg et al., 2020)
  • Uboreshaji wa mifumo ya ekolojia kutawezesha kufanikiwa kufikia Malengo yote 17 ya Maendeleo Endelevu kufikia mwaka unaolengwa wa 2030, ikijumuisha kukomesha umaskini na baa la njaa. (IRP, 2019)

 

UMUHIMU WA MIFUMO YA EKOLOJIA

  • Nusu ya Pato la Taifa duniani hutegemea mazingira na kila dola inayowekezwa katika uboreshaji wake huzalishia uchumi faida ya dola 30. (Verdone and Seidl, 2017)
  • Misitu hutoa maji ya kunywa kwa theluthi moja ya miji mikubwa duniani; pia hutegemewa na asilimia 80, asilimia 75 na asilimia 68 ya spishi zote za amfibia, ndege, na mamalia mtawaliwa. (HLPE, 2017Vié, Hilton-Taylor and Stuart, 2009)
  • Takribani watu bilioni 2 wanategemea sekta ya kilimo kwa maisha yao, haswa watu maskini na watu wanaoishi vijijini.(WRI, 2019)
  • Maeneo ya mboji huhifadhi asilimia 30 ya gesi ya ukaa kutoka mchangani kote duniani. (Scharlemann et al., 2014)
  • Miti barabarani hupunguza joto angalau kati ya nyuzijoto 0.5 hadi 2.0 msimu wa joto, kwa manufaa ya watu karibu milioni 68.  (MacDonald et al., 2016)

 

UHARIBIFU WA MIFUMO YA EKOLOJIA

  • Uharibifu wa mifumo ya ekolojia tayari unaathiri maisha ya watu angalau bilioni 3.2 - asimia 40 ya idadi jumla ya watu ulimwenguni. (IPBES, 2018)
  • Kila mwaka, ulimwengu hupoteza hekta milioni 10 za misitu - eneo lenye ukubwa unaolingana na Jamhuri ya Korea, au Costa Rica mara mbili. (FAO and UNEP, 2020)
  • Mmomonyoko wa udongo na aina nyingine za uharibifu zinagharimu ulimwengu zaidi ya dola trilioni 6 kwa mwaka kukadiria chakula kilichopotea na huduma zingine za mifumo ya ekolojia. (Sutton et al., 2016)
  • Takriban asilimia 30 ya mifumo ya ekolojia ya maji safi imeangamia tangu mwaka wa 1970.
  • Theluthi moja ya akiba ya samaki ulimwenguni wanatumiwa kupita kiasi, zaidi ya asilimia 10 katika mwaka wa 1974. (FAO, 2020)

 

ATHARI ZA UHARIBIFU WA MIFUMO YA EKOLOJIA KWA MAISHA YA BINADAMU

  • Karibu dola trilioni 10 za Pato la Taifa zinaweza kupotea kufikia mwaka wa 2050 iwapo huduma za mifumo ya ekolojia zitaendelea kudidimia. (Johnson et al., 2020)
  • Uharibifu wa ardhi unaweza kupunguza uzalishaji wa chakula ulimwenguni kwa asilimia 12, na kusababisha bei ya chakula kupanda kwa asilimia 30 kufikia mwaka wa 2040.  (ELD, 2015)
  • Inakadiriwa kuwa watu wapatao milioni 700 wanatarajiwa kuhama kutokana na uharibifu wa ardhi na mabadiliko ya tabianchi kufikia mwaka wa 2050. (IPBES, 2018)
  • Kupungua kwa rutuba mchangani katika mashamba ya mahindi hugharimu wakulima nchini Marekani wastani wa dola nusu bilioni  kwa mwaka kupitia mbolea zaidi. (Jang et al., 2020)
  • Uharibifu wa mifumo ya ekolojia unaweza kuongeza maingiliano kati ya wanadamu na wanyamapori na imehusishwa na mkurupuko wa magonjwa. (HLPE, 2017)

 

FURSA NA MANUFAA YA UBORESHAJI

  • Fursa za uboreshaji zinaweza kutokea kwenye hekta bilioni 2 za ardhi iliyokatwa misitu na ardhi iliyoharibiwa kote ulimwenguni - eneo kubwa kuliko Amerika Kusini. (WRI, 2011)
  • Kukidhi lengo la Bonn Challenge la kurejesha misitu kwenye hekta milioni 350 za ardhi iliyoharibiwa na misitu kukatwa kote ulimwenguni kunaweza kuzalisha hadi dola trilioni 9 kama faida. (Verdone and Seidl, 2017)
  • Uboreshaji kupitia kilimo mseto pekee kuna uwezo wa kuimarisha utoshelezaji wa chakula kwa watu bilioni 1.3. (Smith et al., 2019)
  • Kurejesha miamba ya matumbawe Mesoamerica na Indonesia kunaweza kuzalisha zaidi ya dola kati ya bilioni  2.5 na 2.6 kwa mwaka kutokana na huduma za mifumo ya ekolojia. (ICRI, 2018)
  • Uboreshaji wa misitu na mifumo mingine iliyoharibika ya ekolojia ya maji kunaweza punguza gharama ya maji katika miji mikubwa duniani kwa dola milioni 890 kila mwaka, gharama za kuwekea maji dawa ili kuyasafisha. (Shemie and McDonald, 2014)